Salamu za Okwi kwa wana Simba
Kupitia ukurasa wa Twitter aliyekua mfunga mabao hatari wa Simba, Emmanuel Okwi ametuma salamu zake
na ujumbe uliosomeka “Napenda kutangaza kwamba nimejiunga na timu ya SenderjyskE Fodbold ya Denmark na nimesaini mkataba wa miaka mitano.
Namshukuru sana kocha wangu mpya, Jakob Michelsen ambaye ameniangalia nikicheza zaidi ya mechi 20 na kunileta hapa kuwa sehemu ya mafanikio ya timu.
Nawashukuru sana mashabiki wa timu ya Simba na timu ya Taifa ya Uganda ‘The Cranes’ ambao siku zote wamekuwa wakinisapoti na kunihamasisha nifanye vizuri zaidi. Nimefurahishwa sana na salamu za kheri mnazonitumia kupitia mitandao mbalimbali, siwezi kuwajibu wote, lakini mfahamu tu kwamba nahisi mapenzi yenu kwangu.
Naamini kwamba ili kufanikiwa katika maisha, ni vizuri kuondoka vizuri sehemu uliyotoka. Kwa kuzingatia hili, najua kwamba naanza changamoto mpya na wakati huu ni Ulaya.
Salamu za Okwi kwa wana Simba
Reviewed by Steve
on
Saturday, July 11, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Saturday, July 11, 2015
Rating:

