Mnaomwita Mgosi ni mzee, amewaambia hivi....
Siku chache baada ya mshambuliaji mpya wa Simba, Mussa Hassan ‘Mgosi’ kuanza mazoezi na kikosi
cha timu hiyo, amesema anakerwa na wale wanaomuita mzee.
cha timu hiyo, amesema anakerwa na wale wanaomuita mzee.
Mgosi aliwahi kuitumikia Simba lakini baadaye akatimka na kuitumikia Mtibwa Sugar msimu uliopita ambapo alionyesha kiwango kizuri.
Kutokana na hali hiyo, Mgosi amesema kuwa wote wanaomuita jina hilo atawajibu uwanjani wakati akiitumikia Simba katika michuano ya Ligi Kuu Bara msimu ujao.
Akizungumza mshambuliaji huyo alisema kuwa amekuwa akikerwa sana na jina hilo.
“Wanaoniita mzee waache waendelee kuniita jina hilo, lakini namuomba Mungu anijalie uzima ili niweze kuwajibu kwa vitendo nitakapokuwa uwanjani nikipambana na wachezaji wao wanaowaita vijana.
“Najiamini kuwa bado nipo vizuri na ninaweza kupambana kama msimu uliopita ambapo hao vijana wao nilikuwa nikiwakalisha kila wakati, pia nawaomba mashabiki wa Simba wasivunjike moyo na maneno hayo, Mungu yupo na atawajibu uwanjani,” alisema Mgosi.
Mnaomwita Mgosi ni mzee, amewaambia hivi....
Reviewed by Steve
on
Wednesday, July 01, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Wednesday, July 01, 2015
Rating:
