Mkwasa afunguka haya kuhusiana na kauli ya Rais Kikwete
Kauli iliyotolewa hivi karibuni na Rais wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete wakati akihutubia Bunge akieleza
sababu za kutohudhuria uwanjani kuitazama timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ imejibiwa na kocha mkuu wa Stars Charles Boniface Mkwasa akimuomba Mh. Rais kurejea tena uwanjani kuishuhudia timu ya Taifa itakapokuwa ikicheza mechi zake.
Mkwasa amesema kuwa ameguswa na kauli ya Rais na anamwalika rasmi aanze kuhudhuria uwanjani kuishuhudia Stars mpya huku akiahidi kutomwangusha.
“Speech ya Rais Mh. Jakaya Mrisho Kikwete wakati anafunga Bunge kwamba alikuwa ni mmoja wa wadau wa Taifa Stars na maranyingi alikuwa akishiriki lakini bahati mbaya timu imekuwa inafungwa na mpaka ikihamia Zanzibar bado inafungwa, sasa mimi nimeguswa sana na nimetafakari sana mimi nataka kumjibu kwamba Stars sasa imebadilika sio kama zamani”, amesema Mkwasa.
“Kwa kauli yake ile naona kama bado silaha zake ziko begani, kwahiyo mimi ningemuomba kwanza aweke chini aungane na watanzania ambao wameunga mkono timu ya Taifa kwahiyo tuwe nae”, ameongeza.
“Ninamuomba Septemba 5, mwaka huu aje uwanjani tuna mechi kubwa kwahiyo achukue fursa hiyo kuja kuanza kuangalia ‘new’ Taifa Stars kwa maana hiyo hatuta mwangusha kwa maandalizi ambayo tumeyapanga na programu tuliyoiweka naamini kikosi kitakuwa vizuri na siku ya mechi hatutamwangusha”, amesisitiza.
“Tunatumia fursa hii kumwalika rasmi aje aangalie hiyo mechi na ikiwezekana kwakuwa shughuli zitakuwa zimepungua basi awe mdau wa kuweka kiti maalumu kila timu inapocheza awepo uwanjani”, alimaliza.
Awali kwenye hotuba yake ya kulihutubia Bunge mjini Dodoma Mh. Kikwete alisema, amekuwa akihudhuria mechi kadhaa wakati Stars ikicheza lakini kila alipokwenda uwanjani timu hiyo ilishindwa kufanya vizuri hadi kufikia watu kuhisi huenda anamkosi na timu hiyo.
Mkwasa afunguka haya kuhusiana na kauli ya Rais Kikwete
Reviewed by Steve
on
Wednesday, July 15, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Wednesday, July 15, 2015
Rating:
