Propellerads

Man United kumtengea Pauni mil 35 Lewandowski




Imeripotiwa kua kwa sasa Man United imemtupia jicho mshambuliaji wa Bayern Munich, Robert Lewandowski ili
kuziba nafasi ya Robin Van Persie.

Kocha Louis van Gaal anaonekana kuvutiwa na nyota huyo na anataka kumnasa ili awe mbadala wa Van Persie aliyetimkia Fernebahce.

Wakala wa Lewandowski, Cezary Kucharski, anaamini kua klabu hiyo ya Bavaria haina nia ya kumuuza mshambuliaji wake.

"Nadhani itakua ni ofa kubwa sana, sio chini ya Euro mil 50 (pauni mil 35).

"Robert ni miongoni mwa washambuliaji wenye thamani sana sokoni mwenye uhakika wa magoli, assists, na kujituma. Ameonesha hayo kwa miaka mingi katika career yake" Alisema wakala huyo.

"Kila mwaka anakua katika kiwango kizuri na anacheza kwa level za juu sana, hii ni muhimu kwa vilabu vingine kwani ana uwezo mkubwa na uhakika wa mabao walau 30 kila msimu"

Red Devils walionesha kumhitaji Lewandowski tangu akiwa Borussia Dortmund, lakini wakala wake Kucharski hana imani kama mtu wake anaweza kujiunga Premier Leaguer majira haya ya kiangazi.

Man United tayari wametumia kiasi cha pauni mil 80 kwa usajili msimu huu kwa kuwanasa Morgan Schneiderlin, Memphis Depay and Matteo Darmian wakiungana na Bastian Schweinsteiger.
Man United kumtengea Pauni mil 35 Lewandowski Man United kumtengea Pauni mil 35 Lewandowski Reviewed by Steve on Wednesday, July 15, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.