Habari mbalimbali za usajili Ulaya leo
Katika habari za usajili Ulaya leo nimekulete zile zinazowahusu nyota
Angel Di Maria, Zlatan Ibrahimovic, Arturo Vidal, Gonzalo Higuain, Stevan Jovetic, Edin Dzeko, John Stones na Wojciech Szczesny.
Zlatan haondoki sababu ya Di Maria
Di Maria yuko karibu kukumilisha dili lake PSG, mmiliki wa klabu Nasser Al Khelaifi na mkurugenzi wa michezo, Olivier Letang wako London kukamilisha deal, hata hivyo imethibitishwa kua Zlatan Ibrahimovic hataondoka klabuni kama ilivyodaiwa.
Vidal njiani kwenda Munich
Artulo Vidal ameripotiwa kua yuko njiani kwenda Munich kwa ajili ya vipimo vya afya. Bayern Munich tayari walishafanya makubaliano ya dili la Vidal ambalo ni Vidal tu hajaweka saini. Nyota huyo ameweka ujumbe kwenye mitandao ya kijamii kua muda si mrefu atatua Munich.
Man City wnamfukuzia Higuain
Man City wanadaiwa kumfukuzia mshambuliajia wa Napoli, Gonzalo Higuain. Edin Dzeko anatarajiwa kuelekea Roma, huku Stevan Jovetic naye akikaribia kufanya vipimo vya afya Inter, hivyo City wanahitaji kuongeza nguvu ya ushambuliaji kutoka kwa Higuain. Hata hivyo inadaiwa Napoli hawawezi kumwachia Higuain bila kiasi pungufu ya £45 million…
Man United nao wanamfukuzia John Stones
Mashetani wekundu nao wanadaiwa kuingia katika mbio za kumnasa beki wa kati wa Everton, John Stones ambaye kocha Mourinho nae anajipanga kumuwekea dau jingine baada ya lile la kwanza kukataliwa. Kwa sasa inaonekana Mourinho anatakiwa afanye kweli kwani beki huyo anaweza kunaswa na Man Utd.
Szczesny kufanya vipimo vya afya Roma
Gollikipa wa Arsenal, Wojciech Szczesny amewasili Italia kwa ajili ya vipimo vya afya Roma kwa ajili ya kuichezea klabu ya Roma kwa mkopo wa muda mrefu.
Kwingineko
Mshambuliaji wa Ghana Jordan Ayew amemfuata ndugu yake England na kujiunga na Aston Villa kwa dau la £9 million. Nyota huyo anajiunga Aston Villa kwa mkataba wa miaka mitano akitokea Lorient
Habari mbalimbali za usajili Ulaya leo
Reviewed by Steve
on
Tuesday, July 28, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Tuesday, July 28, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment