Propellerads

Usajili unaotarajiwa kutisha Ulaya.




Katika kuelekea dirisha la usajili Ulaya zimesikika tetesi nyingi huku zikiwahusisha wachezaji wakubwa kama vile
Ronaldo, Aguero na wengine kibao.
Leo nakuletea  wachezaji nyota watano ambao wanatarajiwa kua habari kubwa katika uhamisho wao.

Paul Pogba
Bado haijawa wazi kua ni wapi mfaransa huyu ataelekea, lakini tetesi zinazidi kuenea kua ataondoka Juventus. Tayari vilabu vikubwa kama Barcelona, Real Madrid na Paris Saint Germain wameonesha nia ya kuiwania saini ya mkali huyo ambapo Man City nao hawapo nyuma kumuwinda Pogba.
Inadaiwa usajili wa Pogba unaweza kua wa pesa ndefu, kiasi cha pauni mil. 70 hadi 100.

Cristiano Ronaldo
Ripoti za hivi karibuni zinadai Paris Saint Germain wako katika mbio kubwa kumnasa mkali huyu kutoka Ureno, hali ya sasa klabuni Real Madrid inawapa nafasi kubwa zaidi PSG. Pia siku kadhaa zilizopita ilidaiwa wakala wa Cr7 alikua England ambapo alifanya mazungumzo na klabu yake ya zamani Manchester United pia hata Chelsea. 

Sergio Aguero
Nyota huyu kutoka Arjentina  msimu huu amekua mchezaji muhimu zaidi na msaada mkubwa kikosi cha Manchester City msimu huu, kwa sasa inadaiwa kua Real Madrid wana mpango wa kumchezesha La Liga ambapo habari zinazidi kudai kua Madrid wako tayari kumtengea kiasi cha pauni mil. 64, lakini hata hivyo mpaka sasa hapajafanyika rasmi mazungumzo yoyote.

David De Gea
Mlinda mlango wa Manchester United amekua ni target kubwa ya Real Madrid kwa wakati huu, ambapo klabu inatafuta kipa wa kudumu atakaekamata nafasi ya mkongwe Iker Casillas. Kama ukifanikiwa itakua ni miongoni mwa usajili mkubwa Ulaya.


Gareth Bale
Mkali huyu wa Wales amekumbana na kukosolewa sana klabuni Real Madrid mpaka wengine kufikia kudai amechangia matokeo yasiyoridhisha kwa timu msimu huu. Tayari vilabu mbali mbali vikubwa kama vile Manchester United, Manchester City na Bayern Munich vimeripotiwa kuiwinda saini yake, lakini kuna uelekeo mkubwa huenda Bale akarejea tena ligi kuu ya Uingereza msimu ujao.


Usajili unaotarajiwa kutisha Ulaya. Usajili unaotarajiwa kutisha Ulaya. Reviewed by Steve on Tuesday, June 02, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.