Propellerads

Umeicheki hii Kipre Tcheche wa Azam alivyotupia uzi wa Yanga!!





Katika pitapita zangu kwenye mitandao ya kijamii nimekutana na picha moja safi ya mshambuliaji hatari wa Azam fc, Muivory Coast, Kipre Tchetche akiwa amevalia jezi ya mabingwa wa soka Tanzania bara, Dar Young Africans.
Tchetche ameonekana akipiga stori na Mrembo aliyeketi pembeni yake, bila shaka wanamwambia jambo nyeti! hahahahah!
Stori ya ndani inasema kwamba kocha aliyerejea Azam fc, Stewart Hall bado anahitaji huduma ya Tchetche, lakini moja ya mabosi wa Azam hawamtaki mchezaji huyo.
Msimu uliopita nyota huyo anayecheza nafasi zote za mbele alikosa mechi nyingi kwasababu za majeruhi, lakini kuna wakati alifungiwa na klabu yake kwasababu ya utovu wa nidhamu.
Hata hivyo Tchetche alishuka  kiwango tofauti na misimu miwili ya nyuma, kitendo kilichowaudhi matajairi wa Azam fc.
Je, kuvaa jezi ya Yanga kunaashiria nini wakati huu wanajangwani wanajipanga kuanza usajili wa kimataifa?
Umeicheki hii Kipre Tcheche wa Azam alivyotupia uzi wa Yanga!! Umeicheki hii Kipre Tcheche wa Azam alivyotupia uzi wa Yanga!! Reviewed by Steve on Tuesday, June 02, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.