Propellerads

Kumbe ugomvi wa Manji na Mengi kuhusu Yanga ulianzia mbali, ingia hapa.




Mpenzi msomaji, katika pita pita zangu mitandaoni nimekutana na hii makala ambayo nimeona si mbaya wewe kama mdau wa soka ukajua kitu hapa, twende sawa

Kwa takribani miaka kadhaa sasa ya hivi karibuni pamekuwepo na mvurugano usio na kichwa wala miguu kwa
wafanyabiashara wakubwa na maarufu hapa nchini Tanzania. Mmoja akiwa ni mtanzania halisi bwana Reginald Mengi na mwingine akiwa ni mtanzania mwenye asili ya Asia Yusuf Mehboob Manji.



 Wawili hawa kama utakumbuka wamekuwa katika bifu zito tokea miaka ile ya 1997 / 1998 ambapo kama mtakumbuka bwana Mengi alikuwa ndiyo mdhamini kama siyo mfadhili mkuu wa klabu pinzani kwangu ( namaanisha Yanga F.C ).
 Lakini uongozi wake unasemekana ulikuwa na misukosuko mingi sana ambayo hata hivyo wachambuzi wa mambo wanasema ilikuwa ikichochewa na bwana Manji ili kumuharibia bwana Mengi na ashindwe kuiongoza au kuwaongoza watani zangu kimpira timu ya yanga F.C .

 Kitu ambacho kwa kiasi kikubwa sana kilifanikiwa ambapo kama mtakumbuka mwaka 1998 hapo wakati wa mkutano wa Yanga pale hotel ya starlight palitokea fujo kubwa mno ambayo ilipelekea mlinzi wa karibu wa bwana Mengi kupigwa na watu waliokuwa wakimkataa bwana Mengi kuendelea kuwaongoza.

 Na nakumbuka sana siku hiyo bwana Mengi ilibidi akimbie na aende kujificha ktk moja ya vyoo pale Starlight ili kujiokoa mpaka pale baadhi ya wazee wenye busara zao na haswa alikuwa ni mzee Msumi alipoenda kumwokoa na kumtoa pale ukumbini .

 Kisha baada ya muda mchache tu Mengi akaachia ngazi kuwa mfadhili na mdhamini wa klabu ya Yanga. nini kiliendelea? mara tu baada ya bwana mengi kujitoa yanga hasa katika nafasi ya ufadhili mkuu inasemekana na yeye alihakikisha kuwa klabu ya yanga haitawaliki na kama mnakumbuka pia kuna wakati fulani hali ya hewa jangwani haswa kipesa ilikuwa ni mbaya sana ambapo ilisababisha timu kufanya vibaya watu kuchapana sana viboko ( kama mnavyowajua watani zangu yanga kwa kuchapa viboko hawajambo ) hivyo kwa kiasi fulani lengo la bwana mengi likatimia.

 Lakini ikumbukwe pia kuwa wakati bwana mengi akifanya hayo huyu bwana manji na yeye alikuwa ameshajipenyeza yanga kikamilifu na akaanza kwa kuwaweka madarakani watu wake haswa tajiri mosha na wengineo akiwepo hata rais wa sasa wa tff bwana malinzi ili wamtengenezee mazingira ya yeye kuja kuingia yanga. na mbinu kubwa ambayo bwana manji aliitumia ni kuwaweka hao vibaraka wake yanga huku tena akiwazunguka kwa kuwafelisha ktk mambo yao ya kiuongozi ili kusudi tu waonekane hawafai na yeye akatafuta watu wa mjini ambao aliwaweka sawa ( kipesa ) kisha wakaanza kumpigia chapuo bwana Manji apewe klabu ya Yanga mpango ambao ulifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana na mpaka leo bado anadunda klabuni yanga huku bwana mengi akiwa haamini alivyozidiwa ujanja na kanjibai / panjuani. uadui uliongezekaje?

 Mara baada tu ya bwana manji kupewa mikoba ya kuidhamini na kuiongoza yanga habari za ndani zinasema kwamba kitendo hicho hakikumfurahisha kabisa bwana mengi hivyo na yeye akaamua sasa atumie vyombo vyake vya habari ambavyo kiukweli ni super brand kwa sasa hapa tanzania ( ukibisha ktk hili utakuwa una lako jambo tu ila ukweli ndiyo huo ).

Ili kummaliza bwana manji na kwa kiasi kikubwa sana bwana mengi alifanikiwa kwani kama mtakumbuka hapo miaka kadhaa tu iliyopita bwana mengi alidiriki hata kujitokeza waziwazi na kumshutumu bwana manji kuwa ni mnyonyaji na haswa ktk lile sakata lililovuta hisia za watanzania wengi la mengi kutaka kuuziwa hotel ya kilimanjaro lakini pakatokea na figisu figisu hapa katikati na ikala kwake huku bwana Manji akihusishwa na uuzwaji wake na hadi kuwa na share hapo.

Hali hii ya chuki za hawa watu ziliendelea na mpaka leo bado hazijakoma na ili kulidhihirisha hilo ni kwamba hapa majuzi tu gazeti la nipashe liliandika habari moja inayohusisha kampuni ya bwana manji ya quality engineering iliyokwepa kulipa kodi kiasi cha shilingi bilioni 9 za kitanzania na hapo hapo bwana manji nae akikaririwa akimtaja bwana manji kuwa ni fisadi, mwizi na mwongo.

Leo hii tena bwana manji na yeye amekuja na mpya kwa kusema kuwa shabiki namba moja wa klabu yanga ni hayati baba wa taifa mwalimu nyerere lakini akasema tena kwa msisitizo kuwa adui namba moja wa klabu ya yanga ni bwana reginald mengi na kwamba amemvumilia kwa mambo mengi tu na sasa amemchoka hivyo anataka kuwe na mdahalo wa wazi kati yake bwana manji na bwana mengi ili kila mmoja aje na uthibitisho wake wa tuhuma anazotupiwa kisha watanzania tupige kura nani kati yao ndiyo mwongo, mfitini, mnafiki na mwizi.

Haya wana Yanga mambo hayo!!
Kumbe ugomvi wa Manji na Mengi kuhusu Yanga ulianzia mbali, ingia hapa. Kumbe ugomvi wa Manji na Mengi kuhusu Yanga ulianzia mbali, ingia hapa. Reviewed by Steve on Monday, June 29, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.