Tetesi: Man United wamshawishi Schwensteiger
Inadaiwa kua Manchester United wameahidi kumpa nafasi ya
kucheza kikosi cha kwanza endapo atajiunga nao majira haya ya kiangazi kulingana na ripoti.
Kiungo huyo wa Bayern Munich katika kipindi hiki cha usajili amekua akihusishwa sana katika kujiunga na mashetani wekundu, huku akiingia miezi 12 ya mwisho katika mkataba wake wa sasa na Bayern.
Schwensteiger mwenye miaka 30 kwa sasa, amekua akipewa ushauri na baadhi ya wakongwe wengine waliopata kuichezea Bayern kua abaki Ujerumani, lakini The Times wamedai ofa hii ya kucheza kikosi cha kwanza inaweza kumvuta Old Traford.
Nyota huyo alipata kufanya kazi na kocha wa sasa wa Man United, Louis van Gaal kipindi akifundisha Bayern miaka ya 2009-11.
Tetesi: Man United wamshawishi Schwensteiger
Reviewed by Steve
on
Monday, June 29, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Monday, June 29, 2015
Rating:
