Simba kumuanika kocha wao muda wowote wiki hii.
Klabu ya ‘Wekundu wa Msimbaz’i Simba imesema inatarajia kumtangaza kocha wao mpya ndani ya
wiki hii ambaye atachukua mikoba ya kocha Goran Kopunovic ambaye alitimkia kwao mara baada ya ligi kumalizika akishindwa kufikia muafaka na klabu hiyo kwa kile kilichodaiwa kuwa, alitaka dau kubwa ambalo Simba SC ilishindwa kumpa.
Afisa habari wa Simba SC Hajji Manara amesema, suala la kocha tayari limesha kamilika na tayari wameshampata kocha mpya lakini kinachosubiriwa ni kumtangaza rasmi pindi mambo yote na taratibu zitakapokuwa zimekamilika.
“Suala la kocha limeshakamilika nadhani ndani ya siku mbili tatu hizi tutamtangaza. Taarifa nyingine inabidi watu wasiwe na haraka, alikuwa Newcastle, Aston Villa au alikuwa wa Man United tusubiri baada ya siku mbili tatu hizi kocha wa Simba atajulikana”, amesema Manara.
“Sisi tunaanza Camp tarehe 1 Julai, kocha tumeshampata jina tutawatajia nimewambia ndani ya siku mbili tatu hizi mtamjua haitazidi, yani wiki hii haitapita mtamjua. Kocha yupo tayari ni kiasi cha kumtangaza tu, tunataratibu zetu za kutangaza jambo ndani ya Simba. Unajua kila taasisi inamfumo wake wa kutangaza jambo, kila taasisi inataratibu zake na sisi tunataratibu zetu”, amefafanua.
“Tumeamua tuliweke hivi maksudi wala hatufanyi kwa bahati mbaya. Tunafanya maksudi tutamtangaza itakapokuwa tumeamua hivyo. Kocha atakuja mzuri, kocha wa uhakika unajua kwanza lazima tufanye hivi, Simba ni klabu kubwa kuna makocha wengi waliomba nafasi hii kwahiyo ilikuwa ni lazima tufanye uchaguzi ulio sahihi. Nadhani tumefanya uchaguzi sahihi, na wao (mashabiki) watafurahiwatapata kocha bora kabisa”, alimaliza Manara.
Juma lililopita mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba Zacharia Hans Poppe alisema tayari wamempata kocha mpya ambaye ni raia wa Uingereza tayari wameshamtumia mkataba, pindi atakapousaini watamuweka hadharani. Lakini bado Simba wameendelea kupiga kalenda zoezi la kumtangaza kocha huyo ambaye mashabiki wengi wa ‘Mnyama’ wanataka kumfahamu.
Simba kumuanika kocha wao muda wowote wiki hii.
Reviewed by Steve
on
Wednesday, June 17, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Wednesday, June 17, 2015
Rating:
