Saint Cazorla: Arsenal tunatakiwa kuimarisha ulinzi msimu ujao.
SAINT CAZORLA ametoa wazo kwa klabu yake ya Arsenal kua wanatakiwa kuimarisha safu ya ulinzi ili
kuhimili mbio za ubingwa msimu ujao.
The Gunners walimaliza nafasi ya tatu msimu uliopita, pia wakafanikiwa kuchukua kombe la FA, shukrani kubwa zawaendee safu yao ya ushambuliaji.
Wachezaji upade wa mbele (forward) kama vile kina Alexis Sanchez, Olivier Giroud, Danny Welbeck na Theo Walcott, pia viungo Mesut Ozil, Aaron Ramsey na Cazorla walikua na mchango mkubwa katika msimu uliopita.
Lakini Cazorla anaamini timu yake inahitaji kuimarisha ulinzi kama inahitaji kuchukua ubingwa ambao mara ya mwisho ilikua ni 2004.
Alisema "Moja ya mambo muhimu ya kufanya msimu ujao, ni kua moja ya timu zenye safu nzuri ya ulinzi.
"Tunahitaji kuhakikisha upande wa nyuma uwe imara, na daima iwe hivyo.
Msimu uliopita tulipoteza point nyingi nyumbani dhidi ya timu ndogo ndogo, kama tunahitaji ubingwa hatutakiwi kupoteza hizo point"
Kwa sasa meneja wa Arsenal, Arsene Wenger ana mpango wa kumsajili kipa mkongwe wa Chelsea, Petr Cech na mshambuliaji kutoka Porto, Jackson Martinez ambaye anadaiwa kutengewa dau la pauni mil. 25.
Saint Cazorla: Arsenal tunatakiwa kuimarisha ulinzi msimu ujao.
Reviewed by Steve
on
Wednesday, June 17, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Wednesday, June 17, 2015
Rating:
