Propellerads

Raul: Ronaldo na messi wana historia tofauti.




Mkongwe wa Real Madrid, Raul Gonzalez anaamini kua nyota Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wako katika
viwango tofauti vya historia.

Mhispania huyo alisongea hayo wakati alipoulizwa kuhusu nyota hao, lakini akaongeza kua japo wana historia tofauti lakini ni ngumu kulinganisah uwezo wao.

"Hili swala la Ronaldo na Messi kwa wale wanaojaribu kufananisha, haielezeki" aliiambia Marca.

"Wako tofauti katika kiwango cha historia"

"Cristiano ni balaa, na mafanikio yote kayapata ndani ya miaka sita tuu, kupata wastani wa magoli 50 kwa msimu, kama mimi ningeishia 20 tu ( huku akicheka)

"Rekodi zipo kila mtu aone japo kwangu hazikua muhimu sana.

"Lakini iko wazi, ndani ya miezi michache Ronaldo atavunja rekodi yangu ( ya ufungaji wa muda wote Real madrid) na ataweza kufunga magoli mengi zaidi.

Huku Messi akiwa amefunga magoli 58 msimu huu na kutoa usaidizi mara 31, Ronaldo yeye msimu huu amefumania nyavu mara 61 na kutoa usaidizi mara 22.
Raul: Ronaldo na messi wana historia tofauti. Raul: Ronaldo na messi wana historia tofauti. Reviewed by Steve on Monday, June 15, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.