Propellerads

Pamoja na kuipa vikombe Barca, kocha Enrique hatarini kuondoka.



Baada kuiongoza Barcelona kutwaa ubingwa wa vilabu bingwa Ulaya (UEFA Champions League), kocha Luis Enrique amesema hana
hakika kama ataendelea kukinoa kikosi hicho.
Enrique amefanikiwa kukiongoza kikosi cha Barcelona kutwaa vikombe vitatu (treble) kwenye msimu huu ambao ni msimu wake wa kwanza  na kuweka historia mpya kwenye klabu hiyo ambayo kwa mara ya mwisho ilichukua vikombe vitatu kwenye msimu mmoja  ikiwa chini ya Pep Guardiola. Lakini klabu hiyo inaweza kutafuta kocha mwingine kwa ajili ya kumrithi Enrique.
Alipoulizwa kama atakuwepo kukiongoza kikosi jhicho kwa ajili ya msimu ujao utakaoanza mwezi Agost mwaka huu, Enrique alisema: “ Hapana, ukweli ni kwamba sina uhakika, lakini kwa sasa ninafuraha”, alisema.
Mafanikio yao yamekuja kwa jinsi ya kushangaza, Barcelona ambao jana usiku wamenyanyua kombe la tano la vilabu bingwa Ulaya kwa kuifunga Juventus kwa goli 3-1 kwenye mchezo wa fainali uliopigwa mjini Barlin Ujerumani. Magoli ya Ivan Rakitic, Luis Suarez na Neymar yalitosha kuipa Barcelona ubingwa wa vilabu bingwa Ulaya.
“Kwasababu huu ni mchezo wetu wa 60 kwa msimu huu na tumeshinda michezo 50 kati ya hiyo. Haya ni mafanikio ya kihistoria kwa msimu huu, kushinda vikombe vitatu”, aliongeza.
“Ulikuwa ni mwaka mgumu lakini nashukuru kwa watu wote ambao walionesha imani kwangu. Walifikiri ninaweza kufanya vizuri nikiwa hapa, ushindi huu nawapa wao”, Enrique alisema.
“Hatukudhani kama tungeweza kushinda mataji matatu. Unajaibu kufanya kazi yako vizuri lakini ukiwa pamoja na kundi la wachezaji hawa ni kazi rahisi”, alimaliza.
Pamoja na kuipa vikombe Barca, kocha Enrique hatarini kuondoka. Pamoja na kuipa vikombe Barca, kocha Enrique hatarini kuondoka. Reviewed by Steve on Monday, June 08, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.