Propellerads

Nyota watano wanaotizamiwa kuondoka Chelsea.




Huku habari za usajili zikizidi kushika kasi barani ulaya, leo nakuletea nyota watano wa klabu ya Chelsea wanaotizamiwa
kuondoka klabuni kipindi hiki cha usajili.

Oscar
Mchezaji huyu mwenye miaka 23 hakua na msimu mzuri na kocha Jose Mourinho, huku kukiwa na asilimia kubwa za kocha mreno kumruhusu Oscar kuondoka. Tayari Inter Milan wameripotiwa kuonesha nia ya mazungumzo na mkali huyo huku ikidaiwa kumtengea dau la pauni mil. 30.

Petr Cech
Baada ya mvutano wa muda mrefu kati ya jose mourinho na Arsene Wenger tayari ishakua wazi kua kipa huyu anaelekea The gunners. Inadaiwa Cech anakaribia kusaini dili ambayo inakadiriwa kua na thamani ya pauni mil. 11.

John Obi Mikel
Kiungo huyo huyu mnaijeria anadaiwa  kutafuta klabu nyingine ambayo ataweza kucheza kikosi cha kwanza, tayari anaripotiwa kukubaliana dili na klabu moja ya Falme za kiarabu (U.A.E) ianayoitwa Al Ain, ambako ataungana na Asamoah Gyan.

Filipe Luis
Beki huyu wa kushoto mbrazil anaripotiwa kutaka kuondoka Chelsea ikiwa ni baada ya kucheza msimu mmoja pekee. Alijiunga na Chelsea akitokea atletico madrid kwa dau la pauni mil. 16 majira yaliyopita ya kiangazi, lakini inaonesha ushindani na Azipillicueta ni sababu ya yeye kuondoka.

Loic Remmy
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 28 hajapata nafasi sana kwa Mourinho, anaweza kuondoka kukpisa Radamel Falcao. tayari Blues wametangaza bei ya pauni mil. 15 huku vilabu vingi England vikionesha kumhitaji.
Nyota watano wanaotizamiwa kuondoka Chelsea. Nyota watano wanaotizamiwa kuondoka Chelsea. Reviewed by Steve on Tuesday, June 23, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.