Propellerads

Nyota huyu wa Chelsea aelezea tofauti kati ya Ronaldo na Messi.




Mlinzi wa Chelsea, Cesar Azpillicueta ameelezea tofauti katika aina ya ushambuliaji kati ya nyota wa Real Madri, Cristiano Ronaldo na mkali wa Barca, Lionel Messi.

Mhispania huyo amefunguka wakati alipoulizwa chaguo lake ni lipi kati ya nyota hao wakali, ambapo alisema wachezaji hao ni ngumu kuwafananisha.

"Sina chaguo, wote ni wazuri" aliiambia Marca.

"Wako tofauti.

"Messi akiweka mpira mguuni ni ngumu kuuchukua, Ronaldo anafunga kutokea sehemu yoyote"

Wakali hao kila mmoja alikua katika makali msimu huu kwa upande wake, Messi akifunga magoli 58 katika michuano yote, huku Ronaldo akiwa na magoli 61.

Messi na Ronaldo wote wako katika kinyang'anyiro cha Ballon d'Or ijayo, huku wengi wakimpa Messi asilimia kubwa za ushindi.
Nyota huyu wa Chelsea aelezea tofauti kati ya Ronaldo na Messi. Nyota huyu wa Chelsea aelezea tofauti kati ya Ronaldo na Messi. Reviewed by Steve on Tuesday, June 23, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.