Propellerads

Nyota watano wanaohusishwa kuhamia Barca na Real Madrid.




Huku dirisha la usajili likikaribia huku Ulaya, leo tunaangalia nyota watano ambao kwa kiasi kikubwa wanahusishwa na
kuhamia vilabu vikubwa vya Hispania, FC Barcelona na Real Madrid.

Soma: Usajili unaotarajiwa kutisha Ulaya

Aaron Ramsey
Mkali huyu mwenye miaka 24 ambae amekipiga Arsenal "The Gunners" kwa misimu saba sasa, amehusishwa kwa kiasi kikubwa kuhitajika klabuni Barca. Ramsey kuhitajika Camp Nou kulizidi kuchagizwa na kocha wa sasa wa Barca, Chris Coleman ambaye ni raia mwenzie kutoka Wales. Coleman alidai Ramsey anafaa kua katika kikosi chake msimu ujao.

Raheem Sterling
Sterling ambae msimu huu alisisitiza kutaka kuondoka Liverpool huku klabu ikionekana kuuhitaji mchango wake lakini hata hivyo kocha Brendan Rodgers anaonekana hana jinsi tena zaidi ya kumwachia. Winga huyo amekua akihusishwa zaidi kutimkia Real Madrid, na kutua kwa Rafael Benitez kama kocha mpya Real Madrid kunampa nafasi kubwa zaidi, kwani Benitez ndiye aliemsainisha Liverpool.

Ilkay Gundogan
Mkali huyu nae anahusishwa kwa kiasi kikubwa kutimkia Barcelona, mkataba wa Gundogan na klabu yake ya sasa unaisha mwakani hivyo Barca wanaweza kumpata 2016.

Sergio Aguero
Mshambuliaji huyu wa Manchester City anadaiwa kutengewa dau la pauni mil. 64 na Real madrid, ingawa alisajiliwa na Man City akitokea Atletico Madrid ambao ni mahasimu wakubwa wa Los Blancos, haitomzuia yeye kuingia klabuni hapo.

Laurent Koscielny
Mfaransa huyu anayekipiga Arsenal anadaiwa kuwindwa na Real madrid kuimarisha safu ya ulinzi. Mpaka sasa Koscielny amekua ni msaada mkubwa katika safu ya ulinzi Arsenal.
Nyota watano wanaohusishwa kuhamia Barca na Real Madrid. Nyota watano wanaohusishwa kuhamia Barca na Real Madrid. Reviewed by Steve on Friday, June 05, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.