Propellerads

Kocha aliyetimuliwa, Nooj kuwaaga watanzania leo.




Baada ya kibarua chake kuota nyasi, Kocha Mart Nooij leo atapata nafasi ya kuwaaga Watanzania.

Nooij atawaaga Watanzania katika mkutano na waandishi wa habari.
Taarifa kutoka TFF zimeeleza kwamba ingawa mkutano wa leo utakuwa kati ya Rais wa Shirikisho hilo, Jamal Malinzi na waandishi wa habari lakini amemshawishi Nooij kuungana naye.

“President ndiye amemueleza Nooij aungane naye kwa ajili ya kuwaaga waandishi angalau.

“Amemkumbusha kwamba walikutana na waandishi siku ya kwanza na alizungumza na Watanzania kupitia waandishi. Hivyo ni vizuri awaage,” kilieleza chanzo.

Kibarua cha Nooij kimeota nyasi baada ya kuchapwa mabao 3-0 na Uganda katika michuano ya kuwania kucheza Chan.


Kabla ya hapo, Stars ilikuwa imechapwa mabao 3-0 na Misri katika michuano ya kuwania kucheza Kombe la Mataifa Afrika maarufu kama Chan.
Kocha aliyetimuliwa, Nooj kuwaaga watanzania leo. Kocha aliyetimuliwa, Nooj kuwaaga watanzania leo. Reviewed by Steve on Tuesday, June 23, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.