Propellerads

Kaseke aona umuhimu wa kua Yanga.




Kiungo mpya wa Yanga, Deus Kaseke, ametamka wazi kuwa, anaishukuru klabu yake hiyo mpya kwani imechangia kwa kiasi kikubwa yeye kuongezwa katika kikosi cha Taifa Stars kinachojiandaa na mchezo dhidi ya Misri.

Kaseke ambaye ametua Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Mbeya City, hivi karibuni aliitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha Stars kinachonolewa na Mholanzi, Mart Nooij, sambamba na wachezaji Said Mohammed, Vincent Andrew ‘Dante’ wa Mtibwa Sugar na Benedict Tinoko wa Yanga.

Kaseke amesema kuwa bila ya Yanga kumsajili, kusingekuwa na uwezekano wa yeye kuitwa Stars kwa sababu mara nyingi kikosi hicho kimekuwa kikiundwa na wachezaji wengi wanaozichezea klabu za Dar, tofauti na mikoani licha ya wachezaji wengi wa timu za mikoani kuwa na uwezo wa kucheza katika kikosi hicho. 

“Kiukweli kabisa napenda kutoa shukrani kwa viongozi wa timu ya Yanga kwa kuweza kuchangia kwa namna moja au nyingine mimi kuitwa katika kikosi cha Stars, kwani bila ya kuwepo hapa (Dar), ingekuwa ngumu kwangu kuwemo katika kikosi hicho, licha ya kuona nina uwezo wa kukitumikia kikosi hicho kwa kipindi kirefu sasa.


“Nahisi kama nisingekuwa Yanga sasa, ningekuwepo Stars kutokana na wachezaji wengi wanaoitwa ndani ya kikosi hiki kutokea katika timu za hapa Dar, tofauti na mikoani,” alisema Kaseke.
Kaseke aona umuhimu wa kua Yanga. Kaseke aona umuhimu wa kua Yanga. Reviewed by Steve on Monday, June 01, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.