skip to main |
skip to sidebar
1. Ada ya kukuza Soka la Vijana.
Kila timu kuanzia sasa inatakiwa kulipa dola
2000 kwa kila pro ili kukuza soka la vijana. Sasa kama timu inao 7, itatakiwa kulipa dola 14.000 ambazo ni zaidi ya Tsh. 32.000.000.
2. Kodi ya Mapato.
Kuanzia msimu huu TRA inaanza kufanya yao katka ada za usajili na mishahara ya pro ambayo ni 18.5% ya kila watakachopokea. Kwa akili ya kawaida tu, kina Okwi, Niyonzima, Kipre na Twite hawatakubali mpunga waliozoea kupokea kupungua hivyo mzigo wote utaenda kwa timu.
3. Kibali Cha Kufanya Kazi Nchini.
Immigration humpa Pro yoyote anayekuja kufanya kazi nchini kibali ada yake ni dola 600 kwa miaka 2. Sasa imagine timu ina pro 7 kocha 2, jumla yao 9 ambapo gharama zao ni dola 5,400 ambazo ni zaidi ya Tsh. 12,420,000 na gharama hizi hulipwa na timu.
Hizi ndizo gharama klabu za bongo huingia zinaposajili wageni.
Reviewed by
Steve
on
Sunday, June 28, 2015
Rating:
5