Propellerads

Alichokisema Pluijm baada ya sare ya Villa.



Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema ndiyo wanatengeneza kikosi na watu wanapaswa
kuvuta subira.
Pluijm aliwatumia karibu wachezaji wake wageni wote kwa ajili ya kuwaangalia katika mechi ya kirafiki dhidi ya SC Villa ya Ugandailiyopigwa jana kwenye uwanja wa Taifa.
“Utaona mechi imeisha kwa sare ya bila kufungana, licha ya kwamba hakukuwa na mabao, tulipata nafasi ya mkwaju wa penati, lakini tukapoteza”, alisema Pluijm.
“Bado tunatengeneza timu na unaona namna vijana walivyoonesha mchezo mzuri”, aliongeza.
“Bado tuna mechi za kirafiki, muda wa mazoezi ambao pia utatupa nafasi ya kujua tuko vipi. Sasa ni mapema sana kujipima kwa kiasi cha kusema tuko vipi. Naweza kusema ulikuwa mwanzo mzuri,” Pluijm alifafanua.
Deus Kaseke, Malimi Busungu na Geofrey Mwashyuya ni wachezaji wapya waliosajiliwa kwenye kikosi cha Yanga kwa ajili ya msimu ujao na jana walipata nafasi ya kucheza na kuonsha kiwango kilichowavutia watu wengi.
Alichokisema Pluijm baada ya sare ya Villa. Alichokisema Pluijm baada ya sare ya Villa. Reviewed by Steve on Sunday, June 28, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.