Propellerads

Hatimaye Liverpool yawazidi kete Man United kwa Firmino.




Liverpool imethibitisha rasmi kumsajili mshambuliaji wa Brazil, Roberto Firmino kutoka klabu ya Hoffenheim kwa dau la paundi milioni 29.
Firmino mwenye miaka 23 amesaini mkataba wa miaka mitano ambao atakuwa akilipwa mshahara wa paundi laki moja kwa wiki na anaungana na Wabrazil wenzake Anfield, Philippe Coutinho na Lucas Leiva
Hata hivyo, Firmino haendi kuchukua vipimo vya afya mpaka Brazil itakapotoka kwenye michuano ya Copa America inayoendelea nchini Chile.
Mshambuliaji huyo anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Majogoo kwa dau kubwa zaidi kihistoria kwani Andy Carroll, alisajiliwa kwa paundi milioni 35 mwezi Januari 2011 
Mkurugenzi mkuu wa Liverpool, Ian Ayre alisafiri mpaka Chile usiku wa kuamkia leo na kukamilisha usajili wa Firmino ambaye alikuwa anawindwa pia na Manchester United.
Hii ndio Tweet ya Liverpoool asubuhi hii:
 are delighted to announce they have signed Roberto Firmino from Hoffenheim, subject to a medical 
Hatimaye Liverpool yawazidi kete Man United kwa Firmino. Hatimaye Liverpool yawazidi kete Man United kwa Firmino. Reviewed by Steve on Wednesday, June 24, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.