Changamoto tano kwa Ronaldo kabla hajaondoka Real Madrid.
Nyota Cristiano Ronaldo, amehusishwa kwa kiasi kikubwa kutaka kuondoka klabu yake ya Real Madrid, lakini kufuatia
nia hiyo ya Ronaldo anakabiliwa na changamoto zifuatazo.
Moja: Kuweka rekodi ya mfungaji bora wa muda wote wa klabu yake katika La Liga. Tamgu ajiunge Los Blancos, Ronaldo amepata kufunga magoli 225 katika La liga ambapo amebakiza mabao matatu pekee kuivunja rekodi ya ufungaji wa muda wote ya Real madrid La Liga ambayo inashikiliwa na Raul mwenye magoli 228.
Mbili: Kua mfungaji wa muda wote katika historia ya klabu ya Real Madrid. Mreno huyo amepata kuifungia klabu yake magoli 313 katika michezo 300 na anahitaji magoli 10 pekee kumfikia Raul na jina lake kuwekwa vitabu vya historia klabuni hapo.
Tatu: Kua mfungaji bora zaidi wa pili katika historia ya La Liga. Kwa sasa yupo nafasi ya sita akiwa na magoli 225 ambapo anahitaji kuongeza matatu tu kuingia tano bora. Alfredo Di Stefano ana 227, raul 228, Hugo Sanchez 234 na Telmo Zarra akiwa na 254.
Nne: Kua mfungaji bora zaidi pekee katika michuano ya klabu bingwa Ulaya. Ronaldo na Messi kwa sasa wote wanaongoza katika historia ya michuano hiyo, wakiwa na 76 kila mmoja, lakini iko wazi kua Ronaldo anataka kumfunika hasimu wake ili avunje rekodi.
Tano: Kua miongoni mwa wafungaji bora zaidi katika miongoni mwa ligi tano kubwa Ulaya katika historia. Mreno huyo kwa sasa ana magoli 309. Real Mdri yakiwa 225 na kwa Manchester yakiwa 84, Yuko nyuma kwa bao moja pekee dhidi ya Dixie Dean (310), magoli nane nyuma ya Steve Bloomer (317), 56 zaidi nyuma ya Gerd Muller , na 57 zaidi nyuma ya Jimmy Greaves ambaye anashikilia rekodi hiyo
Changamoto tano kwa Ronaldo kabla hajaondoka Real Madrid.
Reviewed by Steve
on
Wednesday, June 24, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Wednesday, June 24, 2015
Rating:
