Propellerads

Dau la Man United la pauni mil 35 kwa Ramos lakataliwa.




Manchester United siku za hivi karibuni wameripotiwa kumtengea dau la pauni mil 35 nyota wa Real Madrid Sergio Ramos, lakini hata
hivyo imeripotiwa dau hilo limekataliwa.

Nyota huyo mwenye miaka 29 kw sasa amekua ni lengo la Man United ambapo pia usajili wake unahusishwa na mlinda mlango mlango wa klabu hiyo, Davi de Gea, ambae nae anatarajiwa kuingia Real Madrid.

Mapema wiki hii iliripotiwa kua Man United wanajiandaa kwa uhamisho wa dili nono, lakini kwa mujibu wa Daily Mail dilim hilo limekataliwa na Real madrid.

Klabu zote mbili zinadaiwa kutaka kufanya maamuzi haraka juu ya swala la uhamisho wa nyota hao wawili, yaani De gea na Ramos, ambao kila mmoja anataka kuelekea klabu ya mwenzake.

Ramos kwa sasa anakadiliwa kupokea mshahara wa pauni mil 4 kwa mwaka klabuni Real Madrid ambapo kama akijiunga Manchester United wameahidi kumuongeza mpaka kufikia kiasi cha pauni mil. 6.5 kwa mwaka.

 Kwsa upande wa De Gea kwa sasa inaonekana safari ya Real Madrid inanukia kwani anadaiwa kuiweka sokoni nyumba yake iliyopo  Altrincham.
Dau la Man United la pauni mil 35 kwa Ramos lakataliwa. Dau la Man United la pauni mil 35 kwa Ramos lakataliwa. Reviewed by Steve on Friday, June 26, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.