Chelsea kumnasa mkali huyu atakayerithi mikoba ya Drogba.
Kocha Jose alisema hatafanya sana usajili wa kutisha kwenye kipindi hiki cha usajili kwasababu anaiamini timu yake anachotakiwa kufanya ni kuongezea kidogo tu kwenye gaps atakazo ziona. Sasa kuna taarifa mpya kuhusu usajili wa Chelsea.
Chelsea wanajiandaa kutuma ofa ya paundi milioni 30 kwa straika wa zamani wa Real Madrid Gonzalo Higuain.Gazeti la The Sun limeripoti kwamba kocha Jose Mourinho ametia baraka zake kumnunua mshambuliaji huyo raia wa Argentina ambaye ameifungia Napoli inayocheza Seria A magoli 19 msimu uliopita.
Inafahamika kwamba klabu hiyo ya magharibi mwa London inapambana kuimarisha safu yake ya ushambuliaji kutokana na gwiji wa klabu Didier Drogba kuondoka Stamford Bridge majira ya kiangazi mwaka huu. Kwa miaka michache iliyopita, Gonzalo Higuain amekuwa akihusishwa sana kujiunga na Arsenal lakini dili halijawahi kukamilika. Chelsea pia inahusishwa na kumsajili Mcolombia, Radamel Falcao baada ya kumaliza mkataba wake wa mkopo Manchester United.
Chelsea kumnasa mkali huyu atakayerithi mikoba ya Drogba.
Reviewed by Steve
on
Tuesday, June 09, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Tuesday, June 09, 2015
Rating:
