Propellerads

Baada ya kusaini Arsenal, Cech aaga Chelsea kwa barua hii.


Arsenal wamemsainisha mkataba golikipa Petr Cech kutoka Chelsea, Cech mwenye miaka 33 ametua Emirates Stadium kwa
mkataba wa muda mrefu (undisclosed) baada ya kudumu Chelsea kwa muda wa miaka 11.
Baada ya kumwaga wino kujiunga na Arsenal, Cech ameandika barua ya kuwaaga mashabiki wa Chelsea kwa ushirikiano waliompa kwa kipindi chote alichokuwa anaitumikia klabu hiyo.
Hii hapa ni barua yake….
Sikuwahi kufikiria kama ingekuja kutokea sikumoja nitakuja kusema kwaheri kwenye klabu ya Chelsea. Klabu ambayo ilikuwa moyoni kila sekunde tangu nilipojiunga nayo Julai 2004, timu ambayo nifikiri siku moja ningetukika glovu na viatu vyangu na kumaliza safari yangu ya soka nikiitumikia. Lakini mara zote maisha hayako kama unavyofikiria.
Tangu 2004 imekuwa ni safari ya aina yake yenye mafanikio kuliko changamoto, tumeweza kushinda kila aina ya taji lililopo kenye ligi ya England hali kadhalika yale ya Ulaya na lile kubwa kuliko la vilabu bingwa barani Ulaya. Nikitazama nyuma kwenye mafanikio pamoja na msimu wa 2010, nyuma zaidi kwenye mataji ya 2005 na 2006, ushindi wa vikombe viwili cha EPL na FA najivunia sana hilo. Pamoja kama timu tuliandika historia.
Baada ya kusaini Arsenal, Cech aaga Chelsea kwa barua hii. Baada ya kusaini Arsenal, Cech aaga Chelsea kwa barua hii. Reviewed by Steve on Monday, June 29, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.