Argentina wasonga kwa ushindi wa matuta.
Timu ya taifa ya Argentina imetinga Nusu Fainali ya michuano ya Copa America kwa ushindi wa penalti 5-4 kufuatia sare ya 0-0 dhidi ya Colombia baada ya sare ya 0-0.
Sifa zimuendeee mshambuliaji wa Juventus ya Italia, Carlos Tevez aliyefunga penalti ya mwisho baada ya kurejeshwa Boca Juniors.
Penalti za Colombia zilifungwa na James Rodriguez, Radamel Falcao, Cuadrado na Cardona wakati Muriel, Biglia na walikosa.
Penalti za Argentina zilifungwa na Messi, Garay, Banega, Lavezzi na Tevez, huku Biglia na Rojo wakikosa.
Kikosi cha Argentina kilikuwa; Romero, Zabaleta, Garay, Otamendi, Rojo, Biglia, Mascherano, Pastore/Banega dk77, Messi, Aguero/Tevez dk73 na Di Maria/Lavezzi dk87.
Colombia; Ospina, Zuniga, Zapata, Murillo, Armero, Cuadrado, Mejia, Rodriguez, Ibarbo/Muriel dk86, Jackson/Falcao dk74 na Gutierrez/Cardona dk24.
Argentina wasonga kwa ushindi wa matuta.
Reviewed by Steve
on
Saturday, June 27, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Saturday, June 27, 2015
Rating:





