Propellerads

Aliyemtia dole Cavani atimuliwa.




Klabu ya Mainz imekasirishwa mno na tabia mbaya za beki wake, Gonzalo Jara wiki hii na haihitaji tena kuendelea kuwa naye msimu ujao.
Beki huyo wa pembeni wa zamani wa West Brom amekuwa akichezea timu hiyo ya Bundesliga tangu aondoke The Hawthorns mwaka jana.
Lakini klabu hiyo kwa sasa ipo tayari kumuuza Jara baada ya kuonyesha utovu wa nidhamu katika michuano ya Copa America inayoendelea nchini kwao, Chile. 






Kamera zilimnasa beki huyo mwenye umri wa miaka 29 akimtia dole nyuma Edinson Cavani, Chile ikishinda 1-0 dhidi ya Uruguay katika Robo Fainali Copa America.
Cavani alitolewa kwa kadi nyekundu na Jara ambaye hakuadhibiwa, baadaye alifungiwa kutocheza sehemu yote iliyobaki kwenye mashindano hayo.
Aliyemtia dole Cavani atimuliwa. Aliyemtia dole Cavani atimuliwa. Reviewed by Steve on Saturday, June 27, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.