Tetesi: Chelsea katika mazungumzo na Falcao.
Mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza, Chelsea, wanadaiwa kua katika mazungumzo na mshambuliaji mkolombia
, Radamel Falcao.
Mchezaji huyo yupo AS Monaco kwa sasa baada ya kuichezea Manchester United kwa mkopo wa muda mrefu ambao wamekataa kumpa mkataba wa moja kwa moja.
Hata hivyo kulingana na Sky Sports, Chelsea ni miongoni mwa vilabu vilivyo katika mazungumzo na mshambuliaji huyo ambae hakua katika kiwango chake msimu huu alipokua na mashetani wekundu.
Falcao, mwenye miaka 29, alifanikiwa kufunga magoli manne pekee katika michezo 29 aliyocheza Premier League.
Kuondoka kwa Didier Drogba Chelsea, kumemuacha Mourinho na machaguo ya washambuliaji wawili tu, Diego Costa na Loic Remmy, hivyo Falcao anaonekana kuhitajika kwa kiasi kikubwa.
Hata hivyo Sky Sports wanadai mshahara mkubwa anaohitaji Falcao unaweza kua kikwazo cha mkolombia huyo kutua darajani.
Tetesi: Chelsea katika mazungumzo na Falcao.
Reviewed by Steve
on
Sunday, May 31, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Sunday, May 31, 2015
Rating:
