Kopunovic asema Simba wakimpata huyu atawasaidia sana......soma hapa kujua ni nani
Kocha wa zamani wa
Simba, Goran Kopunovic amesema iwapo Simba watafanikiwa kumnasa Laudit Mavugo,
atatoa msaada mkubwa katika safu ya ushambuliaji.
Akizungumza na mtandao mmoja, Kopunovic amesema Mavugo ni mmoja wa wachezaji wenye kiwango kizuri
katika ushambuliaji.
“Ninaamini ataongeza
chachu ya Simba kuwa na safu nzuri ya ushambuliaji,” alisema Kopunovic ambaye
ndiye alimpendekeza Mavugo raia wa Burundi.
Mavugo sasa ni
mshambuliaji tegemeo wa Vital’O ya Burundi. Pia timu ya taifa ya Burundi na
tayari yuko katika hatua nzuri ya mazungumzo na mshambuliaji huyo.
Kabla Mavugo aliwahi kufanya kazi pamoja na Kopunovic katika kikosi cha Polisi Rwanda.
Kopunovic asema Simba wakimpata huyu atawasaidia sana......soma hapa kujua ni nani
Reviewed by Steve
on
Sunday, May 31, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Sunday, May 31, 2015
Rating:
