Maneno ya Ozil kwa mashabiki wasiomkubali
Nyota wa Arsenal, Mesut Ozil amedai kua baadhi ya mashabiki wa
klabu hawaoni mchango wake uwanjani.
Kiungo huyo Mjerumani mara kadhaa amekuwa akikosolewa kwa mbinu zake, lakini Ozil anahisi kujituma kwake watu hawaoni.
"Matarajio ya mashabiki ni makubwa sana," aliiambia Express.de.
"Baadhi wanapenda aina yangu ya uchezaji, wengine hapana. Daima iko kama hivyo.
"Kama mchezaji, ninajitahidi, kwa sababu najua nitawaweka wana kikosi wenzangu katika hali nzuri. Lakini ikitokea sijafunga goli au hata shuti, watu wengi wanavunjika moyo.
"Muda mwingine nafikiria hawatambui kiasi gani nakimbia na pasi ngapi ninacheza. Kocha anaona perfomance yangu yote na kiukweli maoni yake ni muhimu sana."
Maneno ya Ozil kwa mashabiki wasiomkubali
Reviewed by Steve
on
Tuesday, September 06, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Tuesday, September 06, 2016
Rating:




No comments:
Post a Comment