Guardiola atapoteza mamilioni ya waafrika kwa maamuzi yake, wakala aweka wazi
Pep Guardiola amemtosa nje ya kikosi cha klabu bingwa mchezaji bora wa
Afrika mara nne Yaya Toure na sasa wakala wa mchezaji huyo amedai hii itaigharimu klabu mamilioni ya mashabiki kutoka Afrika.
Toure ni mchezaji pekee wa kigeni kutoswa katika kikosi cha Guardiola, wakala wake aitwaye Dimitri Seluk kwa mara nyingine amemfungukia bosi wa City kwamba mashabiki wengi kutoka Afrika watahamia Man United.
"Watapoteza mamilioni ya mashabiki wengi kutoka Afrika kwa sababu ya maamuzi ya Guardiola," Seluk aliiambia Daily Mail.
"Sasa wataiunga mkono Manchester United. Waafrika wengi wamesema hawataangalia tena mechi za City kwenye TV."
Hii sio mara ya kwanza Toure na Guardiola kukutana kwani kocha huyo Mhispania ndiye alikua sababu kubwa kwa kiungo huyo kuondoka Barca mwaka 2010.
Guardiola atapoteza mamilioni ya waafrika kwa maamuzi yake, wakala aweka wazi
Reviewed by Steve
on
Wednesday, September 07, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Wednesday, September 07, 2016
Rating:




No comments:
Post a Comment