Kwanini Arsenal wanashindwa kuchukua ubingwa wa EPl, Patrick Vieira ameona mapungufu haya
Mkongwe wa Arsenal, Patrick Vieira amedai kua kabu yake hiyo ya zamani bado
hawaoneshi kua kama washindani 'serious' wa taji la Premier League.
Gunners hawajashinda taji la EPL tangu 2004 ambapo mfaransa huyo alikua miongoni mwa kikosi hodari cha Arsenal.
Vieira ambaye kwa sasa yupo na kikosi cha New York City FC katika Major League Soccer anaamini kua Arsene Wenger anatakiwa kuleta wachezaji wenye nguvu na ushindani ili kuondoa ukame wa taji kwa miaka 13.
"Kwenye kizazi chetu, tuikua na wachezaji wazuri na pia wachezaji wengi walikua na nguvu," aliiambia The Mirror "Tulikua na kina Dennis Bergikamp ambaye alikua mzuri, na Thierry Henry ambaye aliweza kumalizia na pia nguvu, pia wachezaji walikua na nguvu na miili kama Sol Campbell na wengine kama Jens Lehman, David Seaman"
"Lakini kwa sasa nahisi wanakosa kitu na hicho kitu ni nguvu. Miaka hii sita iliyopita wamekua kwenye hii hali, Arsenal imekua ni timu ambayo haiwezi kuchukua taji kutokana na jinsi wanavyocheza na wakati huo huo wanakata tamaa kwenye mchezo ambao wanaweza kushinda,"
Arsena wameanza msimu wa 2016/17 kwa point moja katika michezo miwili baada ya kushindwa na Liverpool katika mchezo wa kwanza na sare ya bila kufungana na Leicester City.
Kwanini Arsenal wanashindwa kuchukua ubingwa wa EPl, Patrick Vieira ameona mapungufu haya
Reviewed by Steve
on
Monday, August 22, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Monday, August 22, 2016
Rating:




No comments:
Post a Comment