Propellerads

Imebainika: Kwanini Mourinho anataka Schwensteiger aondoke



Imekua ikivuma kwamba kocha Jose Mourinho amekua akitaka mmoja kati
ya wachezaji wanaolipwa zaidi klabuni hapo kuondoka, na sasa sababu imefahamika.

Bastian Schwensteiger amekua akifanya mazoezi na kikosi cha vijana wa U-21 katika wiki za hivi karibuni na jumatani iliripotiwa kwamba United wanataka kumuuza kwa pauni mil 2 ili kumtoa katika mfumo wa malipo.

Ripoti mpya kutoka The Daily Express imekuja na sababu mpya ambayo inamfanya Mourinho kutaka nyota huyo wa zamani wa Bayern Munich kuondoka.

Pamoja na kuonesha mchango wake msimu uliopita akiwa na majeraha kwa kocha Van Gaal, inadaiwa kua Schwensteiger alikua na matatizo na wachezaji wenzake.

Katika msimu huo wa 2015/16 wachezaji wenzake wanadaiwa kua walimpa ushauri wa kukaza na kupona majeraha yake kuliko kumpa support mke wake Ana Ivanovic katika mashindano yake ya tennis- ushauri ambao aliupuuza.

Hata hivyo siku za hivi karibuni Mjerumani huyo alitangaza katika Twitter kua hatojiunga tena na klabu yoyote ya Ulaya kama akiondoka Old Trafford, hivyo kuibua tetesi kua huenda akatimkia China au MLS.




Imebainika: Kwanini Mourinho anataka Schwensteiger aondoke Imebainika: Kwanini Mourinho anataka Schwensteiger aondoke Reviewed by Steve on Friday, August 26, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.