Propellerads

Huyu mwingine tena kuondoka Man United



Wachezaji kama Bastian Schwensteiger, Marcos Rojo na
Matteo Darmian tayari wakiwa wamehusishwa kuondoka klabuni Manchester United na sasa imefahamika ni nani anayefuatia.

Kocha Jose Mourinho tayari ametumia kiasi cha pauni mil 185 katika dirisha hili la usajili, bado anahitaji kukiweka sawa kikosi chake kufikia saizi inayoweza kupangwa vizuri.

Beki wa kushoto, Cameron Borthwick-Jackson ni mchezaji mwingine anayeondoka Man United ambapo huenda akaelekea Wolverhamton Wanderers kwa mkopo wa muda mrefu.

Beki huyo alicheza michezo 14 kipindi cha Louis Van Gaal msimu uliopita, na hivi karibuni aliongeza mkataba mpaka kufikia 2020.

Hata hivyo Mourinho ameweka wazi kua beki huyo hatakuwemo kwenye mipango yake msimu huu hivyo anatakiwa aende sehemu nyingine ambapoa anaweza kupata namba ya uhakika.


Huyu mwingine tena kuondoka Man United Huyu mwingine tena kuondoka Man United Reviewed by Steve on Monday, August 22, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.