Higuain atupia huku Juve ikiimaliza Fiorentina
Juventus 2-1 Fiorentina
Gonzalo Higuain ameifungia Juventus huku ikishuhudiwa mabingwa hao
wa Serie A wakiizamisha Fiorentina kwa mabao 2-1 jana jioni .
Sami Khedira aliipatia Juve bao lakuongoza katika dakika ya 37 baada ya kuitumia vizuri pasi ya Giorgio Chiellin.
Fiorentina walisawazisha dakika ya 66 kupitia Nikoa Kalinic, hata hivy Higuain alikomelea msumari wa mwisho kwao Fiorentina dakika ya 75 baada ya kupiga shuti la umbali mfupi na kujihakikishia ushindi.
AS Roma 4-0 Udinese
AS Roma wao wameanza kwa kishindo mbio zao msimu huu baada ya kuwanyuka Udinese kwa bao 4-0 katika mchezo wa ufunguzi Stadio Olimpico.
Diego Perotti alifungua karamu ya mabao kwa mkwaju wa penati dakika ya 56 kabla hajaongeza tena dakika ya 76.
Eden Dzeko naye akatupia dakika ya 83 huku Mohamed Salah akihesabu bao lake la kwanza la msimu dakika mbili baadae.
Higuain atupia huku Juve ikiimaliza Fiorentina
Reviewed by Steve
on
Sunday, August 21, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Sunday, August 21, 2016
Rating:




No comments:
Post a Comment