Griezmann amefunguka kwanini anapaswa kua mchezaji bora Ulaya
Nyota wa Atletico Madrid, Antonie Griezmann anaamini kua anastahili
kuchukua tuzo ya UEFA ya mchezaji bora Ulaya mbele ya nyota wa Real Madrid, Gareth Bale na Cristiano Ronaldo.
Mfaransa huyo msimu wa 2015/16 ulikua mzuri zaidi kwake katika klabu na timu ya taifa, akimaliza ligi na magoli 2, akifikia fainali za klabu bingwa za UEFA akiwa na Atletico Madrid huku pia akashinda kiatu cha dhahabu katika Euro 2016.
Griezmann anaamini perfomance yake msimu uliopita inatosha kabisa kumpa tuzo japo anapambana na wakali wengine kama Ronaldo.
"Najivunia kua mshindani, hii inamaanisha nipo katika njia sahihi ya kuelekea pakubwa," aliiambia 24sata.
"Sitaki kuonekana najivuna, lakini nastahili hii tuzo kwa sababu nilikua na msimu bora zaidi klabuni na timu ya taifa.
"Ulikua ni msimu usiosahaulika, kwanza kwenye kabu bingwa na Atletico, halafu Euro na France,
"Bahati mbaya hatukushinda taji, ilikua ni maumivu kwetu na mashabiki wetu."
Mshindi wa tuzo hiyo atatangazwa alhamisi.
Griezmann amefunguka kwanini anapaswa kua mchezaji bora Ulaya
Reviewed by Steve
on
Wednesday, August 24, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Wednesday, August 24, 2016
Rating:




No comments:
Post a Comment