Chelsea kumsaini mlinda mlango wa Dinamo Zagreb
Chelsea wanajiandaa kumsaini mlinda mlango wa kireno
Eduardo kutoka klabu ya nchini Croatia, Dinamo Zagreb huku kocha wa klabu akithibitisha uhamisho huo.
Stopper huyo mwenye miaka 33 alikuemo kwenye kikosi kilichoshinda Euro msimu huu lakini hakucheza akiwa kama mbadala wa Rui Patricio.
Meneja wa Zagreb, Zlatko Kranjcar jumapili hii aliulizwa wakati wa mchezo wa Champions League dhidi ya Red Bull Salzburg ambapo aliulizwa kama utakua ni mchezo wa mwisho wa Eduardo akasema "Ndio nafikiria hivyo. Eduardo amepata nafasi nzuri ya kuelekea kabu kubwa kama Chelsea.
"Alipofika tulipata ulinzi kwenye timu yetu, na katika wakati wangu amelinda goli ipasavyo. Lakini ukweli ni kwamba anaondoka. Kila la heri kwenye klabu yake kubwa."
Chelsea kumsaini mlinda mlango wa Dinamo Zagreb
Reviewed by Steve
on
Monday, August 22, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Monday, August 22, 2016
Rating:




No comments:
Post a Comment