Propellerads

Bale aeleza kwanini hatosahau huu mwaka



Nyota wa Real Madrid, Gareth Bale amefunguka kua
kwanini hatousahau mwaka huu.

Bale ni miongoni mwa wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya, ametoa shukrani kwa wenzake klabuni na timu ya taifa kwa kuchangia mafanikio aliyoyafikia.

"Ni heshima kuwania tuzo hii," aliiambia 24sata.

"Tuzo kama hizi huwezi kushinda mwenyewe, bali ni kwa kucheza kwa timu, kwa hiyo ninawashukuru wenzangu , kote klabuni na timu ya taifa, wakiwa ni sehemu ya hapa nilipofikia.

"Kushinda klabu bingwa na Real Madrid kwangu kilikua ni kitu kikubwa msimu uliopita.

"Ulikua ni msimu mrefu na mgumu, lakini tulipambana na tulitaka kushinda.

"Kwangu ulikua ni msimu mzuri sana, sio klabuni tu. Pia tulikua na fainali nzuri za Euro, kwa hiyo sitausahau huu mwaka."
Bale aeleza kwanini hatosahau huu mwaka Bale aeleza kwanini hatosahau huu mwaka Reviewed by Steve on Thursday, August 25, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.