Ukiacha Mamelodi, Ngoma amepata zal hili jingine Ulaya, ingia hapa...
Maana
Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma raia wa Zimbabwe, mambo yamekuwa
yakizidi kumnyookea sasa timu kutoka nchini Uswiss nayo inamtaka
akafanye majaribio.
Timu
hiyo ya Uswiss imeibuka ikiwa ni siku chache tu baada ya moja ya timu
tajiri nchini Afrika Kusini ya Mamelodi Sundown kuonyesha nia ya
kumpata.
Katibu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha, amesema :
“Hiyo
klabu ya Uswisi inayomtaka Ngoma ni ya
Ligi Kuu Uswisi, hii ndiyo iliyokuwa ya kwanza kumhitaji straika huyu
lakini nimekuwa nikisikia pia taarifa za Mamelodi ingawa hazijafiga
klabu rasmi."
Hata hivyo, Kocha wa Yanga, Hans van Der
Pluijm, ameshasisitiza kutokuwa tayari kumuachia Ngoma aondoke kikosini mwake
kwani ana mpango naye wa muda mrefu katika michuano ya kimataifa.
“Tuna ligi kuu, Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya, unamuachiaje mtu kama Ngoma kwa wakati huu? Ngoma haondoki na sitakuwa tayari kumuachia jueni hivyo,” alisema Pluijm, raia wa Uholanzi.
Ukiacha Mamelodi, Ngoma amepata zal hili jingine Ulaya, ingia hapa...
Reviewed by Steve
on
Saturday, November 28, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Saturday, November 28, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment