Antony Martial amejibu hivi Instagram baada ya jana kutolewa na Van Gaal

Antony Martial amejibu kupitia mtandao wa Instagram baada ya jana kocha
Louis van Gaal kufanya maamuzi ya kushtukiza kumtoa jana usiku.
Huku bado wakiwa na matokeo ya 0-0, mashabiki wa Man United walighadhabika pale Van Gaal alipamua kumtoa Martial kisha kumwingiza Marouane Fellaini dakika ya 65.
Baadae zilisikika sauti za kuzomea kutoka kwa mashabiki kisha mjadala ukahamia kwenye mitandao ya kijamii.
Baada ya mechi United waliibuka na ushindi wa 1-0, Van Gaal aliulizwa kama alisikia kelele za kuzomea.
"Bila shaka nimesikia, mi sio kiziwi " alisema.
"Hayo ni maoni ya mashabiki, lakini baadaye hawataangushwa na maamuzi ya meneja."
Na huko Instagram Martial alikua tofauti na mtazamo wa mashabiki ambapo amejikosoa mwenyewe kiwango chake ambapo ameandika mechi ilikua mbaya kwake "Bad match for me tonight but good win #Workhard."
Martial hajafunga katika michezo minne iliyopita ya Man United.
Antony Martial amejibu hivi Instagram baada ya jana kutolewa na Van Gaal
Reviewed by Steve
on
Wednesday, November 04, 2015
Rating:

2 comments:
Still ni mchezaj mzuri (h)
Still ni mchezaj mzuri (h)
Post a Comment