Simba ilivyokufa mbele ya Prisons leo

Simba imepoteza mechi yake ya pili ya Ligi Kuu Bara ndani ya
mechi saba tu.
Simba ilipoteza mechi yake ya kwanza ikicheza mechi yake ya nne ya ligi ilipokutana na mabingwa watetezi Yanga iliyowachapa bao 2-0.

Ikiwa ugenini, Simba imekubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa wenyeji wake Prisons ya Mbeya ambayo imetoka kupoteza mechi yake kwa kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Stand United.

Timu hizo zilimaliza kipindi cha kwanza kwa sare ya bila bao kwenye Uwanja wa Sokoine, lakini Prisons wakafanikiwa kupata bao katika kipindi cha pili kilichotawaliwa na ubabe na tafrani.
KIKOSI SIMBA:
Agban, Hassan Kessy, Mohammed Hussein’Tshabalala’, Isihaka Hassan, Juuko Murishid, Justice Majabvi, Simon Sserunkuma, Awadh Juma, Pape N'dew, Joseph Kimwaga na Peter Mwalyanzi.
Simba ilivyokufa mbele ya Prisons leo
Reviewed by Steve
on
Wednesday, October 21, 2015
Rating:



No comments:
Post a Comment