Ngoma aukubali mziki wa ligi kuu bongo na hivi ndio alivyosema
Mshambuliaji nyota wa Yanga, Donald Ngoma amesema kwamba Ligi Kuu
Tanzania Bara ina ushindani na ngumu sana.
Hata hivyo, Ngoma raia wa Zimbabwe ameapa kupambana hadi mwisho kuhakikisha anaisaidia timu yake, pia anapata mafanikio zaidi.
“Wakati nakuja nilijua ni ligi yenye ushindani sana, lakini sasa naona ushindani ni zaidi ya vile nilivyofikiria na kila mchezaji anataka timu yake ishinde.
“Ninachofanya ni kuendelea kuzoea mazingira lakini bado ninapambana sana kuhakikisha nafanya vizuri,” alisema Ngoma.
Fowadi huyo wa zamani wa FC Plutnums ya Zimbabwe sasa ni tegemeo la safi ya ulinzi ya Yanga.
Ngoma aukubali mziki wa ligi kuu bongo na hivi ndio alivyosema
Reviewed by Steve
on
Sunday, October 04, 2015
Rating:



No comments:
Post a Comment