Propellerads

Mwadui yawachapa Majimaji nyumbani huku Mgambo wakilazimisha Sare



Mwadui FC imefanikiwa kujiongezea pointi tatu katika Ligi Kuu Bara
baada ya kuichapa Majimaji kwa bao 1-0 ikiwa nyumbani kwao Songea.

Kutokana na ushindi, Kocha Mkuu wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema wachezaji wake walifuata maelekezo na kusababisha kupatikana kwa matokeo hayo.

“Haikuwa kazi lahisi, lakini walijitahidi kufuata maelekezo na tumeweza kushinda.

“Ni jambo la kuvutia na lenye faida kwetu, uwanja pia ulikuwa mbaya sana lakini tunashukuru tumeshinda,” alisema Julio.

KWINGINEKO
Coastal Union ikiwa nyumbani Mkwakwani Tanga dhidi ya wenyeji wengine wa uwanja huo, Mgambo imeshindwa kutamba baada ya kulazimishwa sare ya bila bao.

                                   

Mechi hiyo ilikuwa kali na ya kuvutia lakini hakuna timu iliyoweza kupata bao katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa Mkwakwani, leo.

Msemaji wa Coastal Union, Oscar Asenga amesema si matokeo mazuri kwa kuwa walitaka kushinda.

"Kweli si dalili nzuri kwa kuwa tulitaka kushinda ili kujiweka vizuri.

"Lakini tunaendelea kupambana ili kufanya vema kwa kuwa tunataka kufanya vizuri," alisema Asenga.

Mwadui yawachapa Majimaji nyumbani huku Mgambo wakilazimisha Sare Mwadui yawachapa Majimaji nyumbani huku Mgambo wakilazimisha Sare Reviewed by Steve on Saturday, October 03, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.