Propellerads

Mourinho amuwakia kocha wa Ubelgiji kuhusu Eden Hazard kwenda klabu hii


                                     
Bosi wa Chelsea, Jose Mourinho amemwambia kocha wa
Ubelgiji Marc Wilmots akae kimya kuhusu hatma ya Eden Hazard klabuni hapo, baada ya kukaririwa wiki hii akisema Hazard anapaswa ahamie Real Madrid.

Mchezaji huyo mwenye miaka 24 aliachwa kwenye mechi waliyoshinda 2-0 dhidi ya Aston Villa wiki iliyopita huku akonekana kua katika wakati mgumu kwa kiwango chake.

Wilmost aliripotiwa kumshawishi winga huyo Mbelgiji kufikiria swala la kuhamia kwa wakali wa Hispania ambapo sasa Mourinho anaona kocha huyo anaingilia mambo yasiyo yake.

"Akiwa kwenye timu ya taifa, hua sifungui mdomo wangu kabisa" Mourinho alisema kama alivyonukuliwa na The Mirror.

"Lakini baadhi ya watu hawana utaratibu kama huo wanaongea mchezaji anapokua klabuni. Hilo sio tatizo langu."


Mourinho amuwakia kocha wa Ubelgiji kuhusu Eden Hazard kwenda klabu hii Mourinho amuwakia kocha wa Ubelgiji kuhusu Eden Hazard kwenda klabu hii Reviewed by Steve on Sunday, October 25, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.