Propellerads

Kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa nae aongea kuhusu Anthony Martial




Didier Deschamps amefunguka kua ameshangazwa sana
na jinsi Antony Martial alivyoweza kuyazoea haraka maisha ya Premier League.

Mchezaji huyo mwenye miaka 19 alisajiliwa majira ya joto kwa ada ya pauni mil 36 ambayo ilivunja rekodi kwa wachezaji chipukizi.

Huku wengi walikua na matarajio makubwa  kuona endapo atafikia thamani ya bei hiyo, hata hivyo Martial amefanya kweli kwa kuonesha kiwango cha juu.

Martial tayari ametupia magoli manne kwa Man United msimu huu, ambapo matatu kwa Premier League na moja kwa Capital One Cup.

Na sasa bosi wa timu ya taifa ya Ufaransa Deschamps amesema anashangazwa na mambo anayoyafanya dogo huyo Old Trafford ambapo ni habari njema kwa timu ya taifa.

"Ana uwezo. Kila mtu anashangazwa kwa kile anachokifanya kwa United ambapo ni nzuri kwake na kwetu," aliwaambia waandishi.

"Anastahili kua hapa-ilikua ni rahisi na kila kitu kilichoandikwa na kuongelewa kuhusu yeye.

"Imewanyamazisha baadhi ya watu. Ni kijana, anaweza kua na wakati mgumu wakati mwingine, lakini anaweza kufanya mambo makubwa- alifanya Monaco.


"Sasa anafanya klabuni kwa kiwango kingine kwa hiyo ni rahisi kuangalia perfomance yake. Pamoja na yote ana kipaji."

Kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa nae aongea kuhusu Anthony Martial Kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa nae aongea kuhusu Anthony Martial Reviewed by Steve on Friday, October 02, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.