Propellerads

Kocha Kerr wa Simba aamua kumpongeza Maguli


                                          
Mshambuliaji hatari wa Stand United,  Elius Maguli ana mabao
manane katika Ligi Kuu Bara na ndiye kinara wa ufungaji, Kocha wa Simba, Dylan Kerr, amesema uwezo wa mchezaji huyo ni aibu kwao.

Kabla ya kuanza kwa msimu huu wa ligi kuu, Simba iliamua kuachana na Maguli ambaye amefunga mabao sawa na yale ya timu hiyo, kwa madai kuwa uwezo wake ni mdogo uwanjani.

                                         
                                         
Kerr, raia wa Uingereza, amesema kuwa, Maguli anastahili kupongezwa kwa kile anachofanya uwanjani na mafanikio yake ni aibu kwa Simba ambayo ilimuacha.

“Maguli anafanya vizuri kwa kufunga mabao nane hadi sasa, ni aibu kwa Simba,” alisema Kerr na alipoulizwa inakuwaje anasema aibu kwao wakati naye alishiriki kwenye kumuacha, alisema: “Kusema kweli ni yeye mwenyewe ndiye aliyetaka kuondoka Simba.”

Katika kikosi cha Simba anayeongoza kwa ufungaji ni Hamis Kiiza aliyefunga mabao matano na wengine waliofunga moja-moja ni  Juuko Murshid, Joseph Kimwaga na Justice Majabvi.
Kocha Kerr wa Simba aamua kumpongeza Maguli Kocha Kerr wa Simba aamua kumpongeza Maguli Reviewed by Steve on Saturday, October 24, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.