Propellerads

Theo Walcott anataka kua kama staa huyu mkongwe wa Arsenal



Theo Walcott amefunguka kua angependa kufuata nyayo za
mkongwe Ian Wright.

Wright alikua mkongwe Arsenal baada ya kucheza kwa muda wa miaka saba Highbury ambapo alikua akiongoza kwa rekodi ya ufungaji wa muda wote klabuni hapo kabla ya Thiery Henry kuvunja rekodi yake.

Matokeo ya Capital Cup kwa mechi zilizochezwa jana

Walcott nae amekua akicheza kama winga na pia mshambuliaji lakini amesisitiza anapata hamasa zaidi kutoka kwa Wright.



"Nilimpenda pamoja na staili yake ya uchezaji kwa sababu mara nyingi alicheza akiwa na tabasamu" Walcott aliiambia tovuti rasmi ya Arsenal

"Alifunga magoli mengi na alisababisha hofu kwa mabeki.

"Hakua mtu mrefu sana duniani ila ile pressure aliyoileta kwa mabeki iliwaogopesha sana.

"Ninaweza kujifunza kwa mbio alizokua nazo, uwezo aliokua nao mchezoni na umaliziaji.

"alipokua ndani ya box hakua ana panic, kitu ambacho nimejifunza kwamba unapokua ndani ya box unakua na muda mwingi kuliko unavyofikiria , Alifanya ionekane rahisi sana.

"Amefunga magoli ya kila aina kitu ambacho kinatakiwa kwa mshambuliaji, kuweza kufunga goli lolote.

"Ni miongoni mwa waliomo kwenye vitabu vya historia vya klabu na pia ni shujaa."

Theo Walcott anataka kua kama staa huyu mkongwe wa Arsenal Theo Walcott anataka kua kama staa huyu mkongwe wa Arsenal Reviewed by Steve on Thursday, September 24, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.