Propellerads

Ripoti: Dili la Cavani na Arsenal bado halijafa



Arsenal wameripotiwa kua katika matumaini ya
kumpata Edinson Cavani ikizingatiwa leo ndi mwisho wa dirisha la usajili.

Tetesi zilizopo sasa ni kua kocha Arsene Wenger assubuhi ya leo aliruka na ndege kuelekea Paris ili kufanya dili hilo la Cavani pamoja na mchezaji mwingine kiungo wa PSG  Adrien Rabiot.

Inadaiwa mazungumzo kuhusu dili yalivunjika ambapo Arsenal walishindwa kufikia dau linalotakiwa la  £50m.

Hata hivyo kwa mujibu wa Daily Mail kocha Wenger bado hajakata tamaa na anatarajia kufanya mambo ili kukamilisha dili hilo ndani ya masaa matatu kabla ya kufungwa kwa dirisha.

Mlinda mlango Petr Cech ndie pekee amesajiliwa msimu huu na Arenal huku Olivier Giroud akiwa mshambuliaji tegemeo wa klabu.
Ripoti: Dili la Cavani na Arsenal bado halijafa Ripoti: Dili la Cavani na Arsenal bado halijafa Reviewed by Steve on Tuesday, September 01, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.