'Kubuma' kwa dili la De Gea, kumbe Real Madrid walichelewesha nyaraka
Inadaiwa kua Real Madrid waliwasilisha nyaraka za uhamisho wa
David De Gea dakika 28 baada ya kufungwa kwa dirisha la usajili.
La liga wamethibitisha kua hawakupokea nyaraka kabla ya kufungwa usajili Hispania usiku uliopita, kwa mujibu wa Sky Sports News ilikua ni Los Blancos walioshindwa kukamilisha dili kwa muda.
Man United wao wamedai walipeleka nyaraka kabla ya kufungwa kwa usajili na wanao ushahidi kua dili kwa upande wao lilikua limekamilika.
Gazeti la Marca limedai kua dili hilo sasa limekwama na linaweza kufanyika tena mpaka Januari mwakani.
Mpaka sasa bado haijafahamika endapo Man United au Real Madrid watakata rufaa kwa sababu ya kuchelewa.
'Kubuma' kwa dili la De Gea, kumbe Real Madrid walichelewesha nyaraka
Reviewed by Steve
on
Tuesday, September 01, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Tuesday, September 01, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment