Tetesi: Uhamisho wa De Gea mbioni kukamilika
Mlinda mlango wa Manchester United, David De Gea
ameripotiwa kua katika hatua za mwisho mwisho kukamilisha uhamisho wake kuelekea Real Madrid.
Karibia kipindi hiki chote cha usajili De Gea amekua akihusishwa sana kutaka kwenda Real Madrid na tetesi hizi ndizo zilizomfanya kocha Van Gaal kutomchezesha katika mechi za kuanza msimu huu.
United walikua wanatarajiwa kumuuza kwa dau la pauni mil 35, lakini The Mirror wamedai kua ada hiyo inaweza kushuka mpaka chini ya pauni mil 30 huku usajili huo ukitajwa kukamilika kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili jumanne.
Pamoja na msimamo wa kocha van Gaal kua hawezi kumwachia nyota huyo, taarifa kutoka upande wa De Gea akiwemo wakala wake Jorge Mendes zinadai wamekua na uhakika mkubwa kua dili linakamilika kufikia jumatatu.
De Gea amebakiza mwaka mmoja pekee katika mkataba wake wa sasa na Man United.
Tetesi: Uhamisho wa De Gea mbioni kukamilika
Reviewed by Steve
on
Friday, August 28, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, August 28, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment